

Lugha Nyingine
公告汇总:联通继续停牌 阳光城股东接盘龙净环保
![]() |
Picha iliyopigwa Julai 28, 2025 ikionyesha aina tatu mpya za magari ya Chery kwenye hafla ya uzinduzi mjini Cairo, Misri. (Xinhua/Sui Xiankai) |
CAIRO – Katika hafla iliyofanya jana Jumatatu kwenye Jumba la Makumbusho la Abdeen la Cairo, Misri, Kampuni ya kuunda magari ya Cherry ya China imetoa aina tano mpya za magari ya Arrizo 5 FL, Arrizo 8, Tiggo 7 Pro Max, Tiggo 8 Pro Max, na Tiggo 9 PHEV ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuingia kwenye soko la Misri.
Shen Xiantian, meneja mkuu wa Chery Tawi la Misri, amesema kampuni hiyo ya kuunda magari itaharakisha mpito wake kuelekea uundaji wa magari yenye injini za mseto na teknolojia ya AI, na kushirikiana na wabia na wasambazaji wa kimataifa kuanzisha mtandao wa kimataifa wa mauzo, huduma na uzalishaji.
"Kwa sasa tunaanzisha vituo vinane vya R&D (utafiti na maendeleo), viwanda 10 vya uundaji magari, na vituo vya usambazaji vipuri katika maeneo muhimu duniani," Shen amesema, akiongeza kuwa kampuni hiyo "itaimarisha ubia na wadau wenyeji ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wa mwisho na wabia wa kikanda."
Kwa mujibu wa takwimu za kampuni, Chery iliuza magari zaidi ya 580,000 yenye kutumia nishati mpya mwaka 2024, na kupata ongezeko la asilimia 232.7 kuliko mwaka 2023.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma